1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Urusi na Iran wasaini mkataba wa ushirikiano

17 Januari 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Iran Masoud Pezeshkian wamesainia makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati katika Ikulu ya Kremlin Ijumaa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Iran Masoud Pezeshkian
Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Iran Masoud PezeshkianPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Iran Masoud Pezeshkian wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakatikatika Ikulu ya Kremlin Ijumaa, yanayolenga kuimarisha ushirikiano, katikati ya machungu ya vikwazo vya magharibi.

Kulingana na Kremlin, makubaliano hayo ya ushirikiano wa kina na kimkakati yatagusa maeneo yote kuanzia biashara na kijeshi hadi sayansi, elimu na utamaduni. 

Ziara hiyo ya Pezeshkian inafanyika siku chache kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, aliyeahidi kusimamia usitishwaji wa vita nchini Ukraine na kuchukua msimamo mkali dhidi ya Iran.

Mwanzoni mwa mazungumzo yao, Putin amemwambia Pezeshkian kwamba makubaliano hayo mapya yatatoa msukumo wa ziada kwenye karibu maeneo yote wanayoshirikiana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW