Viongozi waandamizi wa Syria wafanya ziara ya kwanza Saudia
2 Januari 2025Matangazo
Viongozi waandamizi wa Syria waliwasili Saudi Arabia jana Jumatano katika ziara ya kwanza ya kigeni ya watawala wapya wa Kiislamu wa nchi hiyo tangu kupinduliwa kwa rais Bashar al-Assad mwezi uliopita.
Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa ujumbe huo umeongozwa na waziri wa mambo ya nje, waziri wa ulinzi na mkuu wa idara ya ujasusi. Taarifa hiyo imeitaja ziara hiyo kuwa ya kwanza rasmi ya kigeni, kwa mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa Saudia.
Mwezi uliopita, wajumbe wa Saudia walikutana na kiongozi mpya wa Syria Ahmed al-Sharaa mjini Damascus, ambaye kundi lake ndio liliongoza mashambulizi ya waasi yaliyomuondoa madarakani Assad tarehe 8 Disemba.