1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mustakabali wa Gaza wajadiliwa Sharm el Sheikh

13 Oktoba 2025

Viongozi wanakutana Sharm el Sheikh, Misri kujadili mustakabali wa Gaza baada ya vita vya miaka miwili kuliharibu kabisa eneo hilo

Viongozi waliofika Sharm el Sheikh kushiriki mkutano wa kilele wa dunia kuhusu Gaza
Viongozi mbali mbali washiriki mkutano wa kujadili mustakabali wa Gaza Picha: Eliot Blondet/ABACA/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili muda mfupi uliopita katika mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri ambako atashiriki mkutano wa kilele utakaojadili mustakabali wa Gaza.

Kiongozi huyo wa Marekani anajaribu kutia msukumo wa kupatikana amani katika kanda ya Mashariki ya kati baada ya kuitembelea Israel.

Viongozi wakuu 19 wa nchi na serikali wanahudhuria mkutano huo wa Sharm El Sheikh utakaojumuisha pia hafla ya  kusainiwa makubaliano ya amani ya kumaliza vita Gaza.

Miongoni mwa viongozi walioko Misri ni pamoja na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa,Mahmoud Abbas wa mamlaka ya Wapalestina na Waziri mkuu Keir Starmer wa Uingereza pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  na rais wa baraza la Ulaya Antonio Costa.

Kansela wa Ujerumani  Friedrich Merz ambaye pia amekwenda Sharm El Sheikh amesema nchi yake itasimamia utekelezaji wa mpango huo wa amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW