1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi watoa wito kuvaa kibandiko cha Kippa cha Wayahudi

Sekione Kitojo
31 Mei 2019

Leo Jumamosi(01.06.2019) kutakuwa na maandamano mjini Berlin yanayojulikana kama maandamano  ya Al-Quds,ambayo ni  maandamano yanayoelekezwa kuipinga Israel. Lakini pia kutakuwa na maandamano ya kupinga maandamano hayo.

Deutschland Kippa-Träger Symbolbild
Picha: picture-alliance/dpa/B. Roessler

Baraza  la  Wayahudi  nchini Ujerumani linakosoa  kwamba  hayo ni  maandamano ya  propaganda ya  Waislamu  dhidi  ya  Israel kwa  kile wanachokiita kutaka kuupora mji wa  Jerusalem na  kuifuta Israel kutoka katika ramani ya dunia. Al Quds ni  jina  la  Kiarabu  kwa  mji wa  Jerusalem. Wakati wa maandamano  hayo kutakuwa na maandamano  ya kupinga. 

Myahudi aliyevaa kofia ya Kippa mjini BerlinPicha: picture alliance/dpa/M. Hitij

Afisa anayehusika na  kupambana  na  chuki  dhidi  ya  Wayahudi katika serikali  ya  Ujerumani Felix Klein , ametoa  wito  kabla  ya maandamano  kila mtu avae kofi ya Kiyahudi  kama  ishara ya mshikamano  na  Wayahudi  na kupinga  maandamano  ya Al-Quds. Siku chache  zilizopita  hata  hivyo  alisababisha kuwamo  katika  vichwa vya  habari  vya  vyombo  mbali  mbali, pale  alipowaonya  Wayahudi dhidi  ya  kivaa  kibandiko  hicho hadharani  kila  mahali  nchini Ujerumani.

Ukweli  ni  kwamba  idadi  ya  matukio ya chuki  dhidi  ya  Wayahudi inapanda. Takwimu za  kihalifu  zinaeleza  kwamba  mwaka  uliopita matukio 1799  yalifanyika  kuhusiana  na  chuki dhidi  ya  Wayahudi.

Hii ni  karibu  asilimia 20  zaidi ya  mwaka  2017. Klein alitoa matamshi yake  kwa  msingi  wa  matukio  haya ya  kihalifu yakiongezeka  katika jamii bila ya  kudhibitiwa pamoja na matukio ya  kikatili,  na kuwa chachu ya  chuki dhidi  ya  Wayahudi.

Onyo kwa Wayahudi

Klein  amefafanua  kwamba  mtandao  wa  internet  na mitandao  ya kijamii  imechangia  kwa  kiasi  kikubwa, lakini  pia  mwendelezo  wa mashambulizi  ya  kumbukumbu  ya utamaduni wetu.

Mtu mmoja alitumia mkanda kumchapa Mhayudi mjini Berlin ikiwa ni moja kati ya matuikio ya chuki dhidi ya wayahudi nchini UjerumaniPicha: Jüdisches Forum JFDA

Rais wa  Israel  amekasirishwa  na  onyo  alilotoa  Klein na  kukosoa kile  alichosema , kusalimu  amri  kwa  wenye chuki  dhidi  ya  Wayahudi nchini  Ujerumani.

Kwa mara  nyingine  tena  wayahudi  hawana  uhakika  wa  usalama nchini Ujerumani.

Afisa  anayehusika  na  mapambano  ya  kupinga  chuki dhidi  ya wayahudi  katika jamii  ya  Wayahudi  mjini  Berlin  Sigmount Koenigsberg, hayachukulii  matamshi  ya  Klein kama  kusalimu  amri , badala  yake ni  kama  wito wa  kuwa  macho, ambao  pamoja  na  hayo ni  dhaifu  na  kwamba  umetolewa  kwa njia  mabyo  haistahili. Ningetarajia , kwamba aongeze kuwa  kila  kitu  kitafanyika  ili  kila Myahudi  nchini  Ujerumani  na  kila  siku  na  hata nyakati za  usiku anaweza  kuvaa kibandiko  hicho Kippa.

Kwa  hiyo kungekuwa  na  tamko  la  kupambana  dhidi  ya watu wenye chuki  dhidi ya  wayahudi, amesema  Koenigsberg.

Aina ya kofia ya kibandiko cha KiyahudiPicha: picture-alliance/dpa/S. Schuldt

Muda wa kuchukua hatua

Jamii  ya  Wayahudi  nchini  Ujerumani  inaitaka  serikali  ya  Ujerumani kufanya  mazungumzo  nayo. Muda umepita wa kuchukua  hatua , kwa kuwa  wayahudi  katika  baadhi  ya  maeneo  ya  miji  mikubwa  wako katika  hatari,  kwabababu  wanatambulika  kama  Wayahudi, anasema rais wa  baraza  kuu  la  wayahudi, Josef Schuster. Amekwisha  kuwa katika  hali  hiyo  miaka  miwili  iliyopita.

Anakaribisha, hatua  kama  hizo, iwapo ngazi ya  juu  ya  viongozi  wa kisiasa  wataliangalia  kwa  makini, anasema Svhuster.

Mapambano  dhidi  ya  chuki  kwa  wayahudi  ni  lazima  yawe mapambano  ya  jamii  yote, anasisitiza. Hali  ya  matumizi  ya  nguvu ya  kisiasa  inaonekana  kushika  kasi.

Waandamanaji wakipinga dhidi ya chuki kwa wayahudiPicha: picture-alliance/dpa/S. Pförtner

Hata  hivyo maandamano ya  mjini  Berlin  ya  kile  kinachoitwa  al-Quds si  maandamano ya  chuki  dhidi  ya  wayahudi, haya  ni  maandamano yaliyopangwa  kudai  haki  kwa  Wapalestina. Pamoja  na  kudai haki kwa  Wapalestina  lakini bila  kuangalia  upande  wa  pili yanaweza kuwa  pia  chuki  dhidi  ya  Wayahudi.

katika  mjadala  kuhusu  kuvaa  kibandiko  cha  kitamaduni  cha wayahudi Kippa , rais  wa  Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa wito  watu  wote  watakaoshiriki  katika  maandamano  hayo mbadala wavae  kibandiko  hicho , ili  kupambana  na  chuki  dhidi  ya  wayahudi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW