1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visa vya Ebola vyaongezeka kwa kasi

9 Juni 2026

Zaidi ya watu 100 wamefariki kutokana na Ebola DRC. WHO yasema mapigano na mashambulizi dhidi ya wahudumu yanakwamisha udhibiti.

DR Kongo Munigi 2026 |
Mlipuko wa sasa unasababishwa na virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo ambavyo havina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa.Picha: Jospin Mwisha/AFP

Zaidi ya watu 100 wamefariki kutokana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika muda usiozidi mwezi mmoja tangu mlipuko ulipotangazwa. Kufikia sasa, watu 550 wamethibitishwa kuwa wameambukizwa, huku mkoa wa Ituri ukiwa umeathirika zaidi.

Mamlaka za afya zinasema juhudi za kudhibiti ugonjwa huo zinakwamishwa na mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya, migogoro ya silaha, na baadhi ya wananchi kuwa na mashaka na hatua za afya.

Dkt Abdirahman Mahamud, Mkurugenzi wa Operesheni ya Tahadhari na Majibu ya Dharura kuhusu Afya, katika Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema:

"Mlipuko huu unafuatiliwa kwa karibu zaidi katika mkoa wa Ituri, ambako asilimia 94 ya watu wamethibitishwa kuwa wameambukizwa Ebola. Na kudhihirika kwamba idadi ya watu walioambukizwa imeongezeka ni kutokana na kuboreshwa hatua za kuwapima watu kwa sababu sasa tuna maabara iliyokarabatiwa katika eneo la Mongbwalu, iliyo na uwezo mkubwa wa kufanya vipimo."

Mlipuko huu unasababishwa na virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo ambavyo havina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa.

Nchini Kenya, maandamano dhidi ya mpango wa Marekani kujenga kituo cha karantini cha Ebola mjini Nanyuki yamegeuka vurugu, mtu mmoja ameripotiwa kuuwawa baada ya kupigwa risasi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW