1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visa vya kunyongwa Iran vyazidi kwa asilimia 30 mwaka 2023

2 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa unasema Iran inatoa adhabu za kunyonga kwa "kiwango cha kushtusha" ambapo iliwanyonga watu 419 katika miezi 7 ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Raia wa Iran wakiandamana dhidi ya adhabu ya kunyongwa
Raia wa Iran wakiandamana dhidi ya adhabu ya kunyongwa Picha: Allison Bailey/NurPhoto/picture alliance

Akitoa ripoti mpya ya hali ya haki za binadamu nchini Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Antonio Guterres amesema watu 7 walinyongwa kuhusiana na maandamano yaliyotokana na kuuwawa kwa Mahsa Amini.

Amini msichana wa miaka 22 alikamatwa na polisi wa maadili wa Iran waliodai kwamba alikuwa hajavaa hijab yake kwa njia inayostahili.

Msichana wa Kiiran anayedaiwa kupigwa na polisi amefariki

Guterres ameendelea kusema kwamba katika visa vyote saba, afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilipata taarifa kwamba hakuna hata kesi moja iliyoendeshwa kwa njia ambayo ilikidhi viwango vya kimataifa vya sheria ya haki za binadamu. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW