AfyaAfrika Kusini
Visa vya mpox nchini Afrika Kusini vyaongezeka
11 Septemba 2024Matangazo
Wizara ya Afya ilisema mgonjwa huyo ambaye kwa sasa yuko nyumbani akijitenga hakuwa na historia ya hivi karibuni ya kusafiri kimataifa au kuwasiliana na mtu anayeshukiwa au kuthibitishwa kuwa na Mpox.
Tangu mlipuko huo uanze Mei mwaka huu, watu watatu wamefariki kutokana na Mpox nchini humo.
Wizara ya Afya imeendelea kuwasihi watu wote waliotambulika na wanaoshukiwa kuambukizwa, kushirikiana na maafisa wa afya wakati wa uchunguzi ili kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa huo unaoweza kuzuilika na unaotibika.
Tangu homa ya nyani itangazwe kuwa dharura ya afya ya umma duniani, mamlaka ya usimamizi wa mipaka nchini Afrika Kusini ilichukua hatua kadhaa za kuchunguza watu wanaoingia nchini kupitia mipaka na viwanja vya ndege.