1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita dhidi ya Covid-19: Trump abadili timu ya mawasiliano

Ibrahim Swaibu
8 Aprili 2020

Rais Donald Trump amefanya mageuzi katika kikosi chake cha mawasiliano katika Ikulu ya White House, Stephanie Grisham, mkurugenzi wa mawasiliano ameondoshwa kutoka kwa wadhifa na kurithishwa na Kayleigh McEnany.

USA Coronavirus US-Präsident Donald Trump
Picha: picture-alliance/AP Images/A. Brandon

Hatahivyo Grisham, ambaye amehudumu kwa cheo hicho kwa miezi tisa hajawi fanya mkutano wowote rasmi na wandishi wa habari katika kipindi chake cha uwaziri.

Mageuzi hayo yanajiiri wakati rais Trump akikabiliwa na janga kubwa zaidi kuwahi tokea katika kipindi cha uongonzi wake ambapo virusi vya Corona vinazidi kusambaa kote nchini humo.Trump pia ameongeza wafanya kazi wapya kwenye wizara yake ya mawasiliano na habari akipambana na janga la virusi vya Corona.

Virusi hivyo tayari vimesababishwa vifo vya takribani watu 12,000 nchini Marekani na vimebadilisha pakubwa maisha ya raia wa Mareekani na kuyumbisha uchumi wa taifa ambao unatarajiwa kuwa huenda utashuka.

Stephanie Grisham, aliekuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu ameondolewa katika nafasi yake na kurudishwa ofisi ya mke wa rais Melania Trump.Picha: Reuters/C. Barria

Kulingana na afisa wa ngazi za juu ambaye hakutaka kutajwa majina, katika mageuzi mengine pia, msemaji wa makao makuu ya jeshi la Marekani Pentagon, Alyssa Farah atachukuwa majukumu mapya kama mkuu wa mawasiliano maalum ya kimkakati.

Afisa huyo anasema, uamuzi huo bado haujatanganzwa rasmi. Farah ana mahusiano ya karibu kwa ikulu ya White House baada ya kuwahi kufanyakazi kama mkuu wa habari wa Mike Pence na pia kama mkurugenzi wa mawasilianao katika ofisi ya Meadow.

Usukaji wa timu mpya White House

Mnamo siku ya Jumanne, mkewe rais Trump, Melania Trump alitanganza wadhifa mpya wa Grisham kama mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya mama huyo wa kwanza wa taifa hilo.

Melania alieleza kuwa mkuu wa wafanyakazi katika ofisi yake Lindsay Reynolds ambaye amekuwa katika ofisi hiyo kwa miaka mitatu amejiuzulu ili kupata muda na familia yake.

Shirika la habari la Associated Press linaripoti kuwa kuondoshwa kwake Grisham kutoka kwa wadhfa huo, hakujashanganza raia wengi kwani, mara nyingi ameachwa nje tangu mwanzoni mwa janga la virusi vya Corona huku kikosi cha mawasiliano cha jopo la kupambana na Virusi vya Corona kinachoongozwa na makamu wa rais Mike Pence kikiwa katika mstari wa mbele.

Grisham ambaye aliwarithi Sarah Sanders na Sean Spicer kama waziri wa habari na mawasiliano ndiye anakuwa waziri katika historia ya kisasa ya Marekani ambaye utendajikazi wake haujaonekana sana.

Sarah Sanders alikuwa waziri wa habari kabla ya kujiuzulu mwaka uliopita.Picha: Getty Images/J. Raedle

Katika kipindi chake cha miezi tisa ofisini hajawahi kufanya mkutano na waandishi wa habari. Ijapokuwa alikuwa akionenkana mara kwa mara kwenye runinga ya Fox News, alikuwa akiandaa mahojiano yake kwenye studio kukwepa maswali ya wandishi wa habari.

Wachambuzi wanasema kuna changamoto kubwa katika cheo cha uwaziri wa habari wa nchi hiyo hasa hasa chini ya rais Trump ambaye anataka sana kuzungmuza mbele a wandishi habari na kujigamba kama msemaji bora zaidi, wansema, cheo hicho huhitaji waziri kuwa na utiifu wa hali ya juu zaidi.

Katika wiki kadha ziliopita rais Trump amebadilisha taratibu za Ikulu ya White House kuhusu mazungmzo ya kila siku ya na wandishi wa habari. Rais huyo ameonekana akitangulia kuzungungmza na waandishi habari kabla ya maafisa wake, ili kuonyesha kwamba serikali yake inashughulikia pakubwa janga la Corona.

Kayleigh McEnany ambaye ameteuliwa kama waziri wa habari kwa kipindi kirefu amekuwa mtetezi wa rais Trump kwenye runinga.

Anita McBride, ambaye aliwahi kufanya kama mkuu wa wafanyakazi wa mke wa kwanza Laura Bush amesema kuwa kurejea kwake Grisham katika ofisi ya Melani Trump inaonyesha uhusiano wake wa karibu na mke huyo wa rais.

Chanzo: AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW