1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita ya Cameroon iliyosahaulika yawaacha wakimbizi njiapanda

7 Machi 2022

Miaka mitatu iliyopita idadi kubwa ya raia wa Cameroon walikimbilia nchini Nigeria ili kuokoa maisha yao baada ya vita iliyozuka nchini kwao, tukio ambalo wenyewe wamedai limesahaulika na kuzua sintofahamu.

Zypern | Daniel Ejube und Enjei Grace in der UN-kontrollierten Zone
Picha: Philippos Christou/AP/picture alliance

Miaka mitatu iliyopita, Akor Pelkings aliyaacha makaazi yake na kukimbilia magharibi mwa Cameroon, ambako mzozo ulizuka kati ya vikosi vya usalama na waasi wanaopigania taifa huru.

Leo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 ni mmoja wa wakimbizi 70,000 wa Cameroon nchini Nigeria, akishangaa kwa kukata tamaa ni lini wanaweza kurudi.

Hata hivyo kwa upande wao ni miongoni mwa watu milioni moja walioondolewa na mzozo ambao sasa uko katika mwaka wake wa tano lakini bado umesahaulika na hata haujulikani kwa baadhi ya maeneo ulimwenguni.

Soma pia: UN, mashirika ya haki wasifu hatua ya Cameroon kukiri juu ya mauaji ya raia

Ghasia hizo zilianza mwaka wa 2017,wakati wanamgambo walipotangaza kuwa taifa huru katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-magharibi mwa Cameroon katika maeneo ya watu wachache wanaozungumza lugha ya kiingereza katika nchi inayozungumza Kifaransa.

Wakimbizi wa Cameoon Daniel Ejube na Enjei Grace, wakiwa kambini nchini Cyprus.Picha: Philippos Christou/AP/picture alliance

Wanajeshi wanaotaka kujitenga na vikosi vya serikali wameshutumiwa kwa ukatili katika mapigano hayo, ambayo kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linalo shughulikia migogoro (ICG)mapigano hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000.

Gerard Tiko'Or Akenji, ambaye alianzisha ushirika wa kilimo katika kambi inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  la Ogoja, mashariki mwa Nigeria, amesema wao hawakuwa chanzo cha Mashambulizi hayo bali alishangazwa na kukamatwa kwa vijana wengi kutoka  jamii yake na kuongeza kuwa alichukuliwa mara nne tangu kuanza kwa mzozo hadi hatimaye akakimbia March 2019.

Soma pia: Cameroon: Watu 7 wauawa katika maandamano ya wanaotaka kujitenga

Kulingana na kikundi cha kampeni cha Human Rights Watch (HRW) kilisema Mamia ya shule yameshambuliwa huko na Takriban mashambulio hayo yote yalifanywa na vikundi vilivyojitenga vilivyo na silaha ambavyo vinakataa kuruhusu Kifaransa kufundishwa.

Chu Bernice Chang msichana anayeishi katika kambi ya wakimbizi anasema akiwa na Umri wa miaka 21,kamwe hatasahau kwa mara ya kwanza alipojifungulia nyumbani bila msaada wowote, anasema vituo vya afya vilishambuliwa na cliniki katika kijiji chake ilikuwa ikitumika kama kituo cha vyuma vya jeshi la Cameroon.

wakimbizi watoto wa Cameroon wakibeba watoto katika mji wa Agborkim, wilaya ya Etung katika jimbo la Rivers, kusini-mashariki mwa Nigeria, Februari 2, 2018.Picha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Kulingana na Shirika la Kimataifa linalo shughulikia migogoro (ICG) takribani vijiji 250 vimeharibiwa katika vita, likisema vitendo vya aina hii vilitajwa na wakimbizi wengi kama sababu ya watu kuondoka.

Odilia Ntong, mwenye umri wa miaka 50 aliesema Kijiji chake kilishambuliwa zaidi ya mara sita na waliharibu nyumba kwa risasi.

Anasema kwa siku tano alitembea msituni na wanawake wengine tisa, wakiwa na njaa na kulala chini kabla ya kuvuka mpaka na kuingia Nigeria.

Soma pia: Msukumo wa utengano Cameroon watokana na wanaoishi ughaibuni

Ntong sasa anaishi peke yake hukoTakum, mji mdogo mashariki mwa Nigeria, katika chumba kidogo anachokodisha kwa naira 1,500 ($3.60, euro tatu) kwa mwezi.

 Akor Pelkings yeye anasema  idadi ya wakimbizi iliendelea kuongezeka tangu 2017, wakati fedha zinazotolewa na wafadhili zikipungua anasema baada ya miaka mitano ya vita haoni matumaini anasema marafiki zake wengi wamerejea Cameroon na wengine waliuawa pia wengine bado wako msituni.

     

Chanzo: AFP