1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Vita vya Israel-Hamas: Hali eneo la Gaza yazidi kudorora

17 Oktoba 2023

Umoja wa Ulaya unazindua operesheni ya angani ya kusafirisha misaada ya kibinadamu kuelekea nchini Misri ili iifikishe katika Ukanda wa Gaza.

Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa Gaza inakabiliwa na janga la kiafya kutokana na ukosefu wa maji.
Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa Gaza inakabiliwa na janga la kiafya kutokana na ukosefu wa maji.Picha: Middle East Images/ABACA/IMAGO

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema hayo jana Jumatatu.

Tangazo hilo limejiri wakati hali inazidi kuwa mbaya Gaza na mamia ya maelfu ya watu wanaendelea kukimbia kuelekea kusini mwa ukanda huo, huku jeshi la Israel likijitayarisha kwa operesheni mjini humo.

Israel imeapa kuliangamiza kundi la wanamgambo la Hamas baada ya uvamizi wake kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7. Umoja wa Ulaya, Marekani na Israel ni miongoni mwa mataifa kadhaa ambayo hulitaja Hamas kuwa kundi la kigaidi.

Shirika la Afya Duniani limetahadharisha kuwa Gaza inakabiliwa na janga la kiafya kutokana na ukosefu wa maji.

Wakati huo huo, Ujerumani imesema takriban raia wake 3,000 wamerejea nyumbani kutoka Israel, baadhi yao kwa usaidizi wa serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW