1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Vita vya Ukraine: Urusi yaishambulia miji ya Kiev na Odessa

Daniel Gakuba
8 Mei 2023

Urusi imefanya mashambulizi ya anga kuulenga mji mkuu wa Ukraine, Kiev pamoja na mji wa Odessa kusini mashariki mwa Ukraine.

Ukraine Drohnenangriff auf Kiew
Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko, amesema watu watano wamejeruhiwa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, na watawala wa kijeshi wamesema ndege zipatazo 30 zisizo na rubani zimegunduliwa na kudunguliwa katika anga ya mji huo mkuu.

Katika mji wa Odessa, shambulizi la kombora limeharibu ghala la chakula.

Mashambulizi haya yamefanyika wakati Ukraine ikiadhimisha siku utawala wa kinazi wa Ujerumani uliposhindwa, kumbukumbu ambazo nchini Urusi hufanyika tarehe 9 Mei.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW