1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Urusi na Ukraine vyakuchukua sura mpya

24 Septemba 2025

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dimtry Peskov, ameyasema hayo siku moja baada ya Trump kusema Ukraine inaweza kurudisha maeneo yake yote yaliyochukuliwa na Urusi kwa kuwa kwa sasa uchumi wake umedorora.

2025 I  Donald Trump und Volodymyr zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa na mwenzake wa Marekani Donald TrumpPicha: Ukrainian Presidential Press Office/UPI Photo/IMAGO

Ikulu ya Urusi ya Kremlin imesema leo Jumatano kwamba haina chaguo jingine zaidi ya kuendeleza mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine huku ikipinga madai ya rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba haina uwezo huo.

Msemaji wa Ikulu hiyo ya Urusi, Dimtry Peskov, ameyasema hayo siku moja baada ya Trump kusema Ukraine inaweza kurudisha maeneo yake yote yaliyochukuliwa na Urusi ambayo kulingana na kiongozi huyo, uchumi wake kwa sasa umedorora.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwa upande wake ameendelea kusisitiza kwamba mtu pekee anayeweza kubadilisha hali ya mambo katika vita hivyo ni Rais Donald Trump.

"Trump ni mtu anayeweza kuubadili mchezo peke yake, ikiwa atakuwa na uhakika na Ukraine. Na nadhani yuko karibu zaidi na hali hii, na ndiyo sababu kati yetu, ni Trump pekee anayeweza kubadilisha hali. Kwa leo, tunawajua wachache, sio watu wengi sana duniani ambao wanaweza kubadilisha mchezo. Lakini yeye ndiye yuko karibu zaidi na hili" alisema Zelenskyy.

Wakati hayo yakiendelea, Ukraine imeripoti kushambulia kinu cha nishati cha Salavat katika mji wa kati wa Urusi usiku wa kuamkia leo.