VITA VYAKARIBIA KUMALIZIKA-GBAGBO:
5 Desemba 2003Matangazo
ABIDJAN: Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast amesema kuwa katika kipindi cha siku chache zijazo,anataraji kutangaza kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miezi 14 nchini humo vimemalizika.Rais Gbagbo alitoa matamshi hayo baada ya kukutana na viongozi wa kijeshi na waasi mjini Bouake katika eneo lililo mikononi mwa waasi.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka Septemba mwaka jana,baada ya jeribio la kutaka kuipundia serikali kutofanikiwa.Ingawa rasmi mnamo mwezi Julai kulitangazwa kuwa mzozo wa ivory Coast umemalizika,nchi hiyo ambayo ni mzalishaji mkuu wa kakao duniani,bado imetengwa-waasi wakidhibiti eneo la kaskazini na serikali ikitawala sehemu ya kusini.
