1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vizingiti katika juhudi za mageuzi ya Afrika Magazetini

Oumilkheir Hamidou
30 Juni 2017

Vizingiti katika juhudi za mageuzi, Umoja wa ulaya kutumia misaada ya maendeleo kupambana na chanzo cha ukimbizi na vita vya Malawi dhidi ya kipundupindu ni miongoni mwa mada za Afrika magazetini wiki hii

Afrika Solaranalage
Picha: picture alliance/dpa/Godong

Tunaanza na gazeti la Neues Deutschland linalochambua vizingiti vilivyoko katika juhudi za kuanzisha mageuzi ya kimambo leo  katika bara la Afrika. Gazeti linahisi juhudi hizo zinakabiliana na mizozo ya kila aina. Uhaba wa wasomi wenye maarifa na sera za maana za maendeleo ndio kizuwizi cha maendeleo katika nchi nyingi, linaandika gazeti la Neues Deutschland. Afrika inapewa umuhimu mkubwa katika wadhifa wa Ujerumani kama mwenyekiti wa kundi la mataifa 20 yanayoendelea na yale yaliyoendelea kiuchumi G-20. Katika mkutano wa viongozi wa G-20  mwishoni mwa wiki inayokuja mjini Hamburg, mada kuhusu namna ya kulijumuisha bara la Afrika katika soko la dunia na jinsi ya kupunguza pengo lililoko katika jamii zinatarajiwa kugubika mazungumzo hayo. Serikali kuu ya Ujerumani inataraji kwa kuhimiza vitega uchumi, yataibuka pia matumaini mema  na kwa namna hiyo kupunguza wimbi la wakimbizi wanaoelekea Ulaya.

Gazeti  na Neues Deutschland linazungumzia njia kuu zinazojazana na ujenzi wa majumba  makubwa makubwa ya viyoo yaliyogeuka kuwa kitambulisho cha miji mikubwa mikubwa ya kiafrika kuanzia Tunis mji mkuu wa Tunisia hadi Johannesburg nchini Afrika Kusini. Picha hiyo lakini inakinzana na mitaa ya mabanda inayozidi kuongezeka. Mwanya  unazidi kuwa mpana kati ya kati ya miji mikubwa mikubwa inayofuata utamaduni wa Ulaya na wasomi wanmaovutia na teknolojia ya kimambo leo kwa upande mmoja na wakaazi wengineo wanaofuata mtindo wa maisha ya mashambani kwa upande wa pili. Katika wakati ambapo kundi la kwanza linapendelea nchi zao zijiunge na soko la dunia, kundi la pili zinalenga zaidi usalama na kujitegemea. Neues Deutschland linamaliza kwa kusema ufumbuzi wa maendeleo ya kijamii unaanzia katika kuimarisha demokrasia katika sehemu kubwa zaidi barani Afrika.

 Juhudi za kuzuwia wimbi la wakimbizi

Maendeleo ya kiuchumi na juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa sera zinazofungamanishwa na misaada ya maendeleo ya Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika. Gazeti la mjini Berlin, die tageszeitung linamulika uwiano kati ya shida za kiuchumi na mabadiliko ya tabia nchi likizingatia juhudi za Umoja wa ulaya kuhakikisha misaada ya maendeleo inasaidia kupambana na sababu zilinazowafanya waafrika wazipe kisogo nchi zao. Halmashamuri kuu ya Umoja inasimamia miradi 118 inayogharimu Euro bilioni 1.9 kwa mwaka kwa lengo la kupambana na chanzo cha uhamaji. Lakini miradi ya maendeleo na fedha za wafadhili pekee hazitosaidia kitu. Mashirika ya misaada ya maendeleo hayana usemi mkubwa na mara nyingi fedha zinazodhamiriwa  miradi ya maendeleo zinamalizikia katika benki za ulaya."Asia ya Mashariki hawakusubiri misaada kutoka Marekani, benki kuu ya dunia na wengineo, ili kujiendeleza" amenukuliwa Hamzat Lawal  wa shirika lisilimilikiwa na serikali "Connected Development-COPE akisema . Anakosoa tabia ya nchi nyingi za Afrika kupenda kutegemea wengine na kusema hiyo ndio  sababu ya Afrika kuangaliwa kama mtoto mdogo.

Sababu kuu ya wimbi la wakimbizi inasemekana inatokana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi nchini Nigeria. Hata hivyo die tageszetitung linahisi Nigeria sawa na nchi nyengine za Afrika wana njia nyengine zinazoweza kutumiwa kupunguza matatizo ya kiuchumi kwa msaada wa teknolojia na kupunguza wakati huo huo wimbi la wakimbizi kuelekea ulaya.

Malawi yapania kupiga vita maradhi ya kipindu pindu

Mada yezu ya mwisho magazetini inahusiana na juhudi za serikali ya Malawi za kupambana na maradhi ya kipindupindu. Gazeti la Frankfurter Allgemeine linasema katika wakati ambapo maradhi hao yanazidi kuenea katika nchi nyingi za Afrika, nchini Malawi serikali imeanzisha mpango wa kuwachanja watoto kuanzia umri wa miezi 9 hadi miaka 14. Mnamo muda wa wiki moja, watoto karibu milioni nane wameweza kuchanjwa dhidi ya maradhi hayo ambayo pamoja na homa ya malaria ni maradhi yanayoenea kwa kasi zaidi barani Afrika. Juhudi za  Malawi zinaonyesha kuleta tija linaandika Frankfurter Allgemeine linalotoa mfano wa mkoa wa Nsanje ambako watoto wameanza kuchanjwa tangu mwaka 2015 na kwa wakati huu tulio nao hakuna tena wanaosumbuliwa na maradhi hayo.

 

Mwandishi:Hamidou OummilkheirIBASIS/PRESSER/ALL/PRESSE

Mhariri:Yusuf Saumu