1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen: "Nitapambana na wenye misimamo mikali"

18 Julai 2024

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema yuko tayari "kuongoza mapambano dhidi ya wanasiasa wenye misimamo mikali” wakati akitoa hotuba katika bunge la Ulaya.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen
Ursula von der Leyen asema yuko tayari kukabiliana na misimamo mikali kwenye Umoja wa UlayaPicha: Jean-Francois Badias/AP/picture alliance

Ursula von der Leyen amesema kamwe hatoruhusu watu wenye misimamo mikali kuleta mgawanyiko na kuharibu mtindo wa maisha ya Ulaya.

Ameyasema hayo leo wakati akiomba ridhaa ya wabunge kumpa nafasi ya kuhudumu kwa muhula wa pili kama Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya.

Kiongozi huyo ameliambia bunge la Ulaya, ambalo sasa linajumuisha makundi mawili ya mrengo mkali wa kulia kwamba yuko tayari kufanya kazi na watu wote ili kupambana na itikadi kali za kisiasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW