1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Von der leyen kukutana na Macron kabla ya ziara ya China

3 Aprili 2023

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anatarajiwa kukutana kesho na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,kabla ya ziara yao ya pamoja nchini China wiki hii.

Frankreich - EU-Ratspräsidentschaft
Picha: Michel Euler/AP/dpa/picture alliance

Msemaji wa kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya Erid Mamer amesema viongozi hao wawili watajadiliana kuhusu masuala kadhaa ikiwemo vita vya Urusi nchini Ukraine,sekta ya nishati na maandalizi ya  ziara yao ya China itakayojumuisha kuwa na mkutano wa pamoja na rais Xi Jinping.

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Von der Leyen ametowa tathmini kuhusu sera ya China akisema kwamba nchi hiyo imeonesha kuongeza ukandamizaji nyumbani na kuonesha uthubutu zaidi nje ya nchi kwa kuondowa enzi ya mageuzi na kufungua milango na badala yake kuweka enzi ya usalama na udhibiti ambapo makampuni ya Kichina yanatakiwa kuisaidia serikali katika operesheni za ukusanyaji taarifa za kijaasusi.