1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Von der Leyen kupigia debe "ushindani sawa" na China

6 Mei 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema ataliweka mezani suala la "usawa wa kibiashara" na hina atakapokutana na Rais Xi Jinping ambaye anafanya ziara nchini Ufaransa.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.Picha: Jean-Francois Badias/AP/dpa

Akizungumza saa chache kabla ya mkutano wake na rais Xi pamoja na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa unaotarajiwa kufanyika mjini Paris, bibi Von der Leyen amesema ni lazima wafanye kazi pamoja kufikia ushindani ulio sawa na kuondoa mashaka.

Amesema alikwishawahi kumweleza rais Xi kwamba vizingiti vilivyopo sasa kwa makapuni ya Ulaya kulifikia soko la China ni lazima viondolewe.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukiituhumu China kwamba inatumia njia zisizofaa kuzipatia soko bidhaa zake barani Ulaya.

Hivi karibuni viongozi mjini Brussels walitangaza mpango wa kuweka udhibiti kwa vifaa vya matibabu kutoka China kwa madai ya kuuzwa kwa bei nafuu kuliko zinazotengenezwa barani Ulaya. Hatua hiyo iliyokasirisha sana serikali mjini Beijing.