Von der Leyen: Umoja wa Ulaya utasimama na Ukraine
8 Julai 2023Matangazo
Kupitia ujumbe kwa njia ya mtandao wa Twitter aloutuma hii leo ambayo ni siku ya 500 tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake ndani ya ardhi ya Ukraine.Von der Leyen amesema kipindi hicho kimeakisi utayari wa Ukraine kujilinda na mshikamano usioyumba kutoka Umoja wa Ulaya.
Soma zaidi:Umoja wa Ulaya kuisaidia Ukraine kujiunga na Umoja huo
Wakati huo huo rais Volodymyr Zelensky ametumia siku ya leo kuisifu nchi yake kwa kusimama imara dhidi ya uvamizi wa Urusi na kuapa kuwa nchi hiyo kamwe "haitadhibitiwa na wavamizi". Zelensky ametoa ujumbe huo alipokitembelea kisiwa kidogo cha Bahari Nyeusi kinachotajwa kuwa alama ya upinzani wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.