1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von Leyen kuhutubia Bunge la EU baada ya misururu ya vikwazo

10 Septemba 2025

Katika hotuba hiyo masuala kadhaa zikiwemo mada za ushindani, usalama, ulinzi, biashara ya kimataifa na bajeti ijayo ya Umoja huo wa Ulaya yanatarajiwa kuangaziwa katika hotuba hiyo kwa wabunge.

Strasbourg|  Ursula von der Leyen
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula Von Der Leyen akihutubia katika bunge la Umoja huo mjini Strasbourg, Ufaransa.Picha: Pascal Bastien/AP Photo/picture alliance

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anahutubia hii leo Jumatano kuhutubia Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Ufaransa katika hotuba yake kuu ya kwanza ya muhula wake wa pili katika nafasi hiyo.

Katika hotuba hiyo masuala kadhaa zikiwemo mada za ushindani, usalama, ulinzi, biashara ya kimataifa na bajeti ijayo ya Umoja huo wa Ulaya yanatarajiwa kuangaziwa katika hotuba hiyo kwa wabunge. 

Bi Ursula Von der Leyen anatarajiwa kuwashawishi wabunge wa umoja huo kumuunga mkono katika miradi muhimu ya kisera kwa miaka ijayo, ikiwemo kuendelea kuiunga mkono Ukraineinayokabiliwa na vita na kuboresha uwezo wa ulinzi wa nchi za umoja wa ulaya.

Kiongozi huyo raia wa Ujerumani alichaguliwa tena kama rais wa tume hiyo na wabunge mwaka jana lakini tangu wakati huo amekuwa akikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa kisiasa.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW