1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vurugu uwanjani katika pambano kati ya Mali na Togo

28 Machi 2005

Na hatimae mjini Bamako,pambano la dimba kati ya wenyeji Mali na Togo kuania tikiti ya kuingia katika fainali za kombe la dunia kanda ya Afrika lilibidi kusitishwa baada ya maelfu ya mashabiki kuuvamia uwanja.Togo ilikua ikiongoza mawili kwa moja kufuatia bao la ushindi lililoingia wavuni mnamo dakika ya 90 ya mchezo.Polisi imetumia gesi ya kutoa machozi na viboko kuwatawanya mashabiki.Watu wasiopungua 19 wamelazwa hospitali na dazeni kadhaa wengine kujeruhiwa.Katika kundi nambari moja Mali inashika mkia ikiwa na pointi mbili tuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW