Vurugu zimezuka Hong Kong
3 Oktoba 2014Kiasi ya waandamanaji 200, walikubaliana kundi kubwa linalowapinga mjini Mong Kok, baada ya kuanza jaribio la kuondoa kambi ya waandamaji hao ambao wameifanya baadhi ya sehemu za Hong Kong kuwa katika mkwamo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, polisi katika eneo la tukio waliweza kuzitenganisha pande hasimu katika pande mbili tofauti.
Bwana mmoja ambae aliekuwa akilinda kizuizi katika eneo la maandamano alisikika akisema" Turejesheeni Mong Koko yetu, sisi watu wa Hong Kong tunahitaji chakula".
Vurugu kama hizi zilizuka katika eneo la rasi ya Causeway, ambapo ilikadiriwa watu 25 wenye kutaka demokrasi walikabiliana na wanaopinga kiasi ya watu 50. Mmoja kati ya waandamaji hao alikiska akisema kwa sauti "Hii sio demokrasia tunahitaji watoto wetu wapate chakula"
Katika hatua nyingine kiongozi wa Hong Kong Leung Chun-ying alikuabali kufanya mazungumzo na waandamanaji wanaoshinikiza demokrasi na serikali inayoumuunga mkono ya China ikisema haitafyata mkia kutokana na vurugu hizo mbaya kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa.
Leung ambae amekaidi na kupitisha muda wa waandamanaji wa kumtaka ajiuzulu amerejea onyo lake kwamba hatua kali zaidi zitachukuliwa kwa yoyote atake jaribu kuzua au kuyakalia majengo ya ofisi za serikali katika mji huo.
Aliwaambia waandishi wa habari dakia chake kabla muda huo aliopewa kumalizika kwamaba Katibu Mkuu Carrie Lam atakutana na wanafunzi kwa lengo la kujadili mabadiliko ya kisiasa, lakini bila kutoa muda wa utekelezwaji wa hatua hiyo.
Maelfu ya waandamanaji waliingia katika mitaa ya Hong Kong tangu juma lililopita kudai kile walichokiita demokrasia kamili, ikiwemo mfumo huru wa kupiga kura pale utakapowadia wakati wa kuchagua kiongozi wao mpya mwaka 2017.
Maandamano hayo, katika eneo hilo koloni la zamani la Uingereza yanatajwa kuwa makubwa kutokea tangu lirejeshwe katika himaya ya china 1997, yalianza kujitokeza tangu jumapili iliyopita, ambapo polisi waliweza kutumia gesi ya pilipili, mabomu ya machazi na fimba ili kuweza kuwatawanya.
China imekuwa ikitawala Hong Kongo kupita mfumo wa "nchi moja, mifumo miwili" unaowekwa na sheria mama ambayon inaipa Hong Kong uhuru fulani ambavyo havipatikani katika maeneo mengine ya China.
Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP
Mhariri:Yusuf Saumu