1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vuta nikuvute inaendelea nchini Ukraine

8 Aprili 2007

Kiev:

Licha ya maandamano yanayoendelea tangu siku kadhaa sasa,rais VIKTOR JUSCHTCHENKO wa Ukraine anashikilia uamuzi wake wa kulivunja bunge.Katika hotuba yake kupitia televisheni ,rais Juschtschenko amesema uamuzi wake unaambatana na sheria-na machafuko hayatakayotokea kwasababu vikosi vya usalama vitawajibika-amesisitiza rais huyo wa Ukraine.VIKTOR JUSCHTSCHENKO anaeelemea upande wa magharibi anapimana nguvu na waziri mkuu VIKTOR JANUKOWITSCH anaeelemea zaidi upande wa Urusi.Mvutano kati ya viongozi hao wawili umeripuka baada ya baadhi ya wabunge kuihama kambi ya JUSCHTSCHENKO na kujiunga na upande wa waziri mkuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW