1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vikuu Ujerumani vyazindua kampeni kuelekea uchaguzi

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2025

Vyama vikuu vitatu nchini Ujerumani vimezindua kampeni kuelekea uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika mnamo Februari 23.

Olaf Scholz na Alice Weidel
Olaf Scholz | Alice WeidelPicha: Kappeler/Albert/dpa/picture alliance

Vyama vikuu vitatu nchini Ujerumani vimezindua kampeni kuelekea uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika mnamo Februari 23. Wajumbe wa chama cha Social Democratic SPD walikusanyika mjini Berlin, na kumthibitisha Kansela Olaf Scholz kama mgombea mkuu na kupitisha ilani yake ya uchaguzi.

Soma: Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025

Nacho chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, cha mbadala kwa Ujerumani AfD pia, kilikutana Jumamosi katika mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Riesa kwa mkutano wa siku mbili, ambao ulimchagua kiongozi wa chama Alice Weidel kama mgombea wa ukansela katika uchaguzi ujao.

Takriban waandamanaji 10,000 wanaoipinga AfD walichelewesha kuanza mkutano huo baada ya kufunga barabara.

Nayo kamati tendaji ya chama cha kihafidhina ya CDU, ilikutana kuhitimisha mkutano wake wa siku mbili katika jiji la kaskazini mwa Ujerumani la Hamburg.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW