Vyama vya SPD na CDU vyaunda muungano mpya Brandenburg
16 Machi 2026
Makubaliano hayo yaliosainiwa na waziri mkuu wa jimbo hilo Dietmar Woidke wa SPD, pamoja na mwenyekiti wa CDU wa eneo hilo Jan Redmann katika mji mkuu wa Potsdam, karibu na Berlin, yanaweka vipaumbele vya serikali mpya kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu ijayo.
Serikali ya awali iliyoongozwa na SPD ilivunjika mapema Januari baada ya mivutano ya ndani katika chama kipya cha BSW.
Woidke alikataa kuitisha uchaguzi wa mapema na badala yake akaunda muungano mpya na CDU, hatua inayofanana na muundo wa serikali ya kitaifa inayoongozwa na Kansela Friedrich Merz.
Chama cha BSW, kinachojulikana kwa msimamo wake kuikosoa jumuiya ya NATO, kilishindwa kuvuka kizingiti cha asilimia tano katika uchaguzi wa shirikisho mwezi Februari, ingawa kilishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa jimbo hilo mwaka 2024.