1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Vyama vya wafanyakazi vyagoma Ufaransa

18 Septemba 2025

Mgomo na maandamano makubwa yanaendelea nchini Ufaransa , ambapo wafanyakazi wanapinga mipango ya serikali ya kupunguza bajeti.

Ufaransa | Maandamano
Vyama vya wafanyakazi vinaitaka serikali kufuta mipango ya kifedha ya serikali iliyopita, kuongeza matumizi katika huduma za umma.Picha: DW

Walimu, madereva wa treni, wafamasia na wahudumu wa hospitali wameungana na vijana wa shule za sekondari kuonyesha upinzani wao kwa sera za kubana matumizi.

Vyama vya wafanyakazi vinaitaka serikali kufuta mipango ya kifedha ya serikali iliyopita, kuongeza matumizi katika huduma za umma, kutoza kodi zaidi kwa matajiri, na kufuta mabadiliko yasiyopendwa ambayo yanawalazimu watu kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kabla ya kustahili pensheni.

Ghasia hizi zinajitokeza wakati Rais Emmanuel Macron na waziri mkuu mpya, Sebastien Lecornu, wanakabiliwa na mgogoro wa kisiasa na shinikizo la kurekebisha hali ya kifedha katika taifa lenye uchumi wa pili kwa ukubwa ulaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Bruno Retailleau, amesema polisi tayari wameondoa baadhi ya vizuizi, vikiwemo vile vilivyowekwa na waandamanaji mbele ya vituo vya mabasi mjini Paris.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW