1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyanzo: Wapiganaji wa M23 bado wapo katika mji wa Uvira

18 Desemba 2025

Waasi wa M23 na maafisa wao wa kijasusi waliovalia nguo za kiraia bado wanaendelea kuwepo katika mji wa mashariki mwa Kongo wa Uvira.

Uvira | Wapiganaji "Wazalendo" wakikabidhi silaha kwa waasi wa M23
Wapiganaji wa kundi la M23 wakikagua silaha zilizokabidhiwa na Wapiganaji Wazalendo katika mji wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Daniel Buuma/Getty Images

Hayo yameelezwa na vyanzo vya kiusalama katika eneo hilo, baada ya kundi hilo la  waasi wa M23  linaloungwa mkono na Rwanda kutangaza kuwa limeanza kujiondoa katika mji huo na kuahidi kuwa zoezi hilo linatarajiwa kukamilika leo Alhamisi.

Tangu kutolewa kwa tangazo hilo, serikali ya Kongo na hata baadhi ya wakazi wa Uvira wameelezea mashaka yao, wakisema huenda hatua hiyo ni mbinu ya M23 ya kuipotosha jumuiya ya kimataifa, huku wakitoa wito wa tahadhari.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW