1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Waandamanaji Bangladesh wavamia gereza na kuwaachia wafungwa

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Wanafunzi wanaoandamana nchini Bangladesh wamevamia gereza moja leo na kuwafungulia mamia ya wafungwa, wakati polisi wakipambana kutuliza machafuko.

Bangladesh|Dhaka|Maandamano
Maandamano yanayoitikisa Bangladesh yahusisha wanafunzi dhidi ya chama tawala cha Awami League.Picha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Mikusanyiko mikubwa ya watu imeshuhudiwa katika mji mkuu wa Dhaka, licha ya polisi kuipiga marufuku.

Takriban watu 50 wameuawa nchini humo wiki hii baada ya polisi kufanya msako mkali kwa lengo la kuzima maandamano ya wanafunzi wanaotaka marekebisho ya sheria za kuwaajiri watumishi wa umma.

Hospitali ya Chuo cha Madaktari cha Dhaka imesema watu wasiopungua 19 wamefariki katika jiji hilo siku ya Ijumaa. Maandamano hayo ya wanafunzi yamesababisha uharibifu mkubwa wa majengo ya serikali na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti kote nchini.

Miongoni mwa ofisi zilizoharibiwa, ni makao makuu ya shirika la utangazaji la Bangladesh.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW