1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji Georgia wakabiliana na polisi

30 Novemba 2024

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika nje ya bunge la Georgia kwa usiku wa pili mfululizo jana Ijumaa, wakipinga uamuzi wa serikali kusitisha mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Georgia | Maandamano dhidi ya serikali
Waandamanaji wakiwa wamekita kambi mebel ya majengo ya bunge la Georgia mjini Tbilisi.Picha: GIORGI ARJEVANIDZE/AFP

Polisi walitumia mabomba ya maji kutawanya umati, na makabiliano yalizuka katika miji ya Tbilisi na Batumi, ambapo waandamanaji walijaribu kuvunja milango ya bunge na kujenga vizuizi.

Ghasia hizo zinafuatia uchaguzi wenye utata uliofanyika Oktoba 26, ambao ulionekana kama kura ya maoni juu ya uanachama wa Umoja wa Ulaya, na kusababisha maandamano ya upinzani na kususia bunge, huku kukiwa na madai kwamba chama tawala cha Georgian Dream kilighushi uchaguzi huo kwa ushawishi wa Urusi.

Rais Salome Zourabichvili alijiunga na waandamanaji Alhamisi baada ya kuishutumu serikali kwa kutangaza "vita" dhidi ya watu wake yenyewe. Katika hotuba yake ya Ijumaa kwa taifa, Zourabichvili aliwasihi polisi wasitumie nguvu dhidi ya waandamanaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW