1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waandamanaji wachoma majengo ya serikali Bangladesh

Sylvia Mwehozi
19 Julai 2024

Maandamano ya wanafunzi yanayoendelea nchini Bangladesh yamesababisha uharibifu mkubwa wa majengo ya serikali na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti kote nchini.

Bangladesch | Maandamano ya wanafunzi mjini Dhaka
Maandamano ya wanafunzi Bangladesh.Picha: Mohammad Ponir Hossain/REUTERS

Watu wasiopungua 39 wamepoteza maisha, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kufuatia ripoti za makabiliano kwenye nusu ya wilaya 64 za nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na polisi imesema kuwa waandamanaji wamechoma, kuharibu na kutekeleza "shughuli za uharibifu" kwenye ofisi nyingi za polisi na serikali.

Miongoni mwa ofisi hizo, ni makao makuu ya shirika la utangazaji la Bangladesh, Televisheni ya Dhaka, ambayo hadi sasa bado haiko hewani baada ya mamia ya wanafunzi waliojawa na hasira kuvamia jumba hilo na kuchoma moto jengo.

Wanafunzi hao wanataka kukomeshwa kwa mfumo wa ajira serikalini ambao wanasema unayapendelea makundii maalum ikiwemo watoto wa vigogo.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi