Waandamanaji waingia mitaani kupinga wizi uchauzi Msumbiji
18 Oktoba 2023Matangazo
Huku matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa Jumatano wiki iliyopita yakisubiriwa, chama tawala cha Frelimo kimetangazwa mshindi katika miji mingi ambako uhesabuji wa kura umekamilika.
Matokeo hayo yamepingwa na chama kikuu cha upinzani Renamo, ambacho kinadai ushindi hususan mjini Maputo.
Soma zaidi: Machafuko yaibuka Msumbiji, ikisubiri matokeo ya uchaguzi
Akiuhutubia umati wa watu mjini humo, Rais wa Renamo Ossufo Momade alitoa wito kuwataka raia wote wa Msumbiji washiriki maandamano ya kupinga udanganyifu katika uchaguzi akisema huu ni mwanzo wa mapinduzi nchini humo.