1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamarekani waandamana kumpinga Trump na sera ya uhamiaji

31 Januari 2026

Waandamanaji waliendesha mgomo wa "hakuna kazi, hakuna shule, hakuna ununuzi” kote Marekani siku ya Ijumaa kupinga msako wa wahamiaji unaofanywa na utawala wa Trump.

Marekani Minneapolis 2026 | Mwonekano wa angani wa maandamano ya "ICE Out" baada ya ufyatuaji risasi uliosababisha vifo
Marekani Minneapolis 2026 | Mwonekano wa angani wa maandamano ya "ICE Out" baada ya ufyatuaji risasi uliosababisha vifoPicha: Brian Snyder/REUTERS

Baadhi ya shule huko Arizona, Colorado na majimbo mengine zilifuta masomo mapema kwa kutarajia wanafunzi wengi kutohudhuria. Maandamano mengine mengi yalipangwa kwa ajili ya wanafunzi na watu wengine kukusanyika katika vituo vya miji, majengo ya serikali za majimbo na makanisa kote nchini humo.Maandamano hayo, yalifanyika huku kukiwa na hasira kubwa kufuatia mauaji ya Alex Pretti, muuguzi wa wagonjwa mahututi ambaye alipigwa risasi mara kadhaa baada ya kutumia simu yake kurekodi maafisa wa Ulinzi wa Mpaka wakifanya operesheni ya kuwakamata wahamiaji mjini Minneapolis.Kifo hicho kimeongeza ukosoaji kuhusu mbinu za utawala wa Trump, kufuatia kifo cha Januari 7 cha Renee Good, aliyepigwa risasi na afisa wa Uhamiaji na Forodha (ICE) wakati akiwa ndani ya gari lake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW