1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wanaoiunga na kuipinga serikali wapambana Kenya

23 Julai 2024

Waandamanaji wanaoipinga serikali na kundi linaloiunga mkono, wamembana nchini Kenya. Vurugu hizo zimeachangia kuungua moto pikipiki ya ya waliokuwa wakipaza sauti kumuunga mkono rais.

Kenia | Maandamano Nairobi
Waandamanaji wanaoiunga na kuipinga serikali wapambana nchini KenyaPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Kundi hilo linalounga mkono serikali liliingia katika mitaa ya Nairobi pikipiki mapema Asubuhi ikiwa ni kabla ya maandamano yaliyopangwa na
waandamanaji wanaoipinga serikali.

Polisi ya Kenya imeonya dhidi ya maandamano katika eneo la uwanja wa ndege

Kwingineko, polisi walifyatua vitoa machozi kwa waandamanaji ambao waliokuwa wameifunga barabara nyingine kubwa inayoelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa Tume ya Kitaifa ya Kenya Haki za binadamu takriban watu 50 wameuwawa na wengine 413 wamejeruhiwa katika vurugu hizo za maandamano ya tangu Juni 18.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW