Waandamanaji wataka adhabu kali zaidi
30 Novemba 2007Matangazo
Mamia ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Sudan,Khartoum wakilaani adhabu iliyotolewa kwa mwalimu wa Kingereza.Mwalimu Gillian Gibbons ameadhibiwa kifungo cha siku 15 baada ya kufikishwa mahakamani kwa mashtaka kuwa aliitusi dini ya Kiislamu alipowaruhusu wanafunzi wake kutoa jina la Mohamed kwa dubu la sanamu yaani „teddy bear“.Waandamanaji wamesema,mwalimu huyo apewe adhabu ya kifo.