1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi 49 wameuwawa kwa mwaka 2019

17 Desemba 2019

Kwa mujibu wa Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka RSF, takribani nusu ya waandishi wa habari 400 waliofungwa duniani kote wapo katika mataifa matatu tu, ambayo ni China, Misri na Saudi Arabia

Demonstration Journalisten Presse
Picha: picture-alliance/dpa/M. Scholz

Akizungumza kabla ya kuchapisha ripoti ya mwaka huu ya shirika hilo kuhusu uhuru wa habari  mjini Berlin, msemaji wa bodi ya RSF Michael Rediske amesema mataifa hayo yameongeza mbinyo kwa watu wanaofanya kazi katika vyombo vya habari. Kwa mujibu wa RSF, China pekee ina wanataaluma ya habari  wapatao 120 gerezani. Zaidi ya asilimia 40 ni waandishi wa habari raia wa taifa hilo, ambao pamoja na kuwepo kwa udhibiti mkali, wamejaribu kusambaza habari kupitia mitandao ya kijamii.

Idadi ya waliuwawa yapungua ikilinganishwa na mwaka 2018

Mwandishi wa habari wa Palestina aliyejeruhiwa kwa risasiPicha: Getty Images/AFP/A. Momani

Na idadi nyingine kuwa ya wafungwa iliyoongozeka kwa mwaka huu ni jamii ndogo ya Waislamu wa Uighur. Kiasi ya waandishi wa habari 49 na wajuzi wengine katika taaluma ya habari wameuwawa katika maeneo tofauti ya ulimwengu, kutokana na kazi zao tangu mwanzoni mwa mwaka, ambapo zaidi ya nusu ya idadi hiyo ni kutoka mataifa Syria, Mexico, Afghanistan, Pakistani na Somalia.

Aidha dondoo za ripoti hiyo mpya zinaonesha idadi ndogo ya waandishi waliuawa katika maeneo ya migogoro ikilinganishwa na mwaka uliopita. Msemaji wa RSF Rediske anasema taifa kama Mexico ambalo halina vita limekuwa hatari kwa waandishi wa habari kama Syria ambalo lipo vitani. Kulikuwa na vifo 86 katika kipindi kama hichi kwa mwaka uliopita.

Syria na Mexico zaongoza kwa vifo

Kwa kuzingatia mwanzoni mwa mwaka huu hadi Desemba 1, mataifa yaliorikodi vifo vingi ni Syria ambapo watu 10 waliuawa, Mexico 10, Afghanistan 5, Pakistan 4, Somalia watu watatu na Saudi Arabia 3. Na waandishi wingine 13 wameuwawa katika maeneo ya Amerika ya Kusini. Shirika hilo la waandishi wa habari wasio na mipaka hadi wakati huu wanataaluma mbalimbali zaidi ya 389 wapo gerezani. Na asilimia 12 ya hao wamekuwepo humo hata kabla ya mwaka uliopita.

Ripoti inaeleza karibu nusu wa waandishi walioko magerezani wapo China ambayo imewafunga waandishi 120, Misri 34, Saudi Arabia 32. Na Misri na Saudi Arabia wameingizwa magerezani bila ya kufunguliwa mashitaka. Uturuki waandishi kadhaa waliachiwa huru baada ya kumaliza muda wao lakini hata hivyo wapo ambao walikamatwa tena na kurudishwa magerezani.

Na hadi Desemba Mosi wanataaluma katika sekta hiyo ya habari 57 duniani kote wametekwa na hasa Syria, 30, Yemeni 15, Iraq 11 na Ukraine mmoja.