1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Waandishi habari Ugiriki wafanya mgomo wa saa 24

17 Aprili 2024

Chama kikubwa kabisa cha waandishi habari Ugiriki kinafanya mgomo wa sekta zote za habari kwa saa 24. Televisheni na redio za Ugiriki hazikurusha habari zozote na mitandao ya intanet haikuchapisha habari kwenye tovuti.

Mgomo wa waandishi habari Ugiriki
Hakuna habari zilizochapishwa katika vyombo vyote nchini Ugiriki kwa saa 24Picha: Nikolas Kokovlis/NurPhoto/picture alliance

Chama kikubwa kabisa cha waandishi habari nchini Ugiriki kinafanya mgomo wa sekta zote za habari kwa saa 24. Televisheni na redio ya Ugiriki haikurusha habari zozote na mitandao ya intanet haikuchapisha habari kwenye tovuti zao. Mgomo huo ulitangazwa kuanzia saa kumi na moja kamili Jumanne asubuhi na ukamalizika saa kumi na moja kamili asubuhi ya Jumatano.

Soma pia: Serikali ya Ugiriki yakabiliwa na shinikizo la kuondolewa

Hatua hiyo inajiri kabla ya mgomo wa siku nzima uliopangwa na Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Ugiriki, ambao unatarajiwa kuathiri huduma za usafiri wa umma.

Muungano huo ulisema unachukua hatua dhidi ya kile ulichokiita mazingira magumu kabisa ya kazi na mishahara ya chini sana. Umesema mishahara yao haitoshi kuyakidhi mahitaji ya msingi ya familia na ya kibinafsi. Kupanda kwa mfumuko wa bei kumeifanya hali kuwa mbaya zaidi. Gazeti la kila wiki la Athens To Vima lilitathmini kuwa bei za bidhaa zimepanda kwa asilimia 37 katika miaka miwili iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW