1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wa habari Afrika waaswa kuwasaidia wananchi

Veronica Natalis
2 Mei 2022

Waandishi wa habari barani Afrika wametolewa mwito wa kuhakikisha wanasaidia wananchi kunufaika na rasilimali zao, taofauti na ilivyo sasa ambapo kunashuhudiwa vifo na mapigano hasa katika nchi zenye rasilimali nyingi.

Symbolbild Whistleblower Afrika
Picha: Andrey Popov/Panthermedia/imago images

Wito huo umetolewa na waziri wa habari wa  Tanzania Nape Nauye, katika maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele chake siku ya Jumanne.

Katika maadhimisho haya yanayozihusisha nchi takribani 10 za bara la Afrika, waziri wa habari wa Tanzania  Nape Nauye ,  pamoja na mambo mengine amewaambia waandishi wa habari kwamba wanalo jukumu kubwa la kutumia taaluma zao  na kuhahakikisha wanaisaidia Afrika kunufaika na rasilimali zake kama vile madini, ardhi, mito maziwa na bahari, akisema Afrika ni Tajiri na haipaswi kuendelea kuwa kama ilivyo sasa.

 Akizungumzia upande wa majukumu ya serikali ya Tanznaia katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza waziri Nape amebainisha kuwa, kwa sasa kuna mabadiliko makubwa yanayofanyika kupitia wizara yake ya habari akitaja mchakato wa  marekebisho ya sheria ya  huduma za habari  ya Tanzania ya mwaka 2016, pamoja na kanuni zake za mwaka 2017, kama mfano wa kushughulikia matatizo yanayoikumba sekta ya habari nchini Tanzania.

Waandishi wa habari wa CongoPicha: Ju Huanzong/Xinhua/imago images

Katika mawasilisho ya mada mbali mbali za washiriki kutoka nchini nyingine barani Afrika, imeonekana kwamba kumekuwa na matatizo makubwa ya uhuru wa habari kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwepo, wamiliki wa vyombo vya habari mitandaoni kulazimishwa  kuondoa maudhui yao mitandaoni, mashambulizi ya kimtandao katika baadhi ya nchi, pamoja na kuminywa kwa uhuru wa watu kutoa maoni au kujieleza hasa katika kipindi cha uchaguzi. Nje ya ukumbi wa mikutano, katibu mkuu wa baraza la habari Tanzania Kajubi Mkajanga,pamoja na kusifu juhudi za serikali ya Tanzania kwa sasa za kuonesha mwanya wa kuwepo kwa uhuru wa kujieleza lakini anakosoa baadhi ya mambo. Waandishi wa habari mjini Bukavu waandamana kupinga ukatili dhidi yao

Miongoni mwa mada zinazojadiliwa  katika maadhimisho haya, ni pamoja na uandishi wa habari na changamoto za kidijitali, matumizi ya teknolojia katika kulinda uhuru wa vyombo vya habari pamoja na kujenga mshikamano wa waandishi wa habari wa bara la Afrika. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni uandishi wa habari na changamoto za kidijitali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW