1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanahabari mjini Bukavu waandamana kupinga ukatili dhidi yao

Mitima Delachance10 Desemba 2021

Waandishi habari wa mkoa wa Kivu Kusini wanafanya maandamano mjini Bukavu kulaani kile wanachokiita kuwa ukatili unaofanywa na vyombo vya usalama dhidi yao.

Symbolbild I Kivu See im Ost Kongo
Picha: Pamela Tulizo/AFP/Getty Images

Ni mamia ya wanahabari walioandamana kwenye barabara ya Patrice Emery Lumumba mjini Bukavu ili kuonesha hasira zao. Wakiwa wamevaa nguo nyeusi, wanahabari hao wamefikisha malalamiko yao kwenye ofisi ya gavana kule Labotte ndani ya mtaa wa Ibanda, wakimtaka ajihusishe katika kulinda haki ya upashaji habari kivu kusini.

Desemba tarehe 2, waandishi habari tisa walikuwa wahanga wa unyanyasaji na dhuluma zilizo wanywa na polisi dhidi yao mjini Bukavu pale polisi walipozuia kikao cha bunge cha kumtimua gavana wa kivu kusini kisifanyike. Wakati huo, wanahabari watatu waliumizwa vibaya.

Kiongozi wa muungano wa waandishi habari wa Congo katika mkoa wa kivu kusini, UNPC, Darius Kitoka, ameitaka serikali kutumia kubeba dhamana na kuhakikisha   vitendo vya ukatili dhidi ya wanahabari havirudiwi tena.

Kuwajibisha wahusika

Wakati wa kupokea barua ya malalamiko ya wanahabari, waziri wa mambo ya ndani na usalama kivu kusini ambaye pia ni ndiye gavana kwa muda, ameomba radhi kwa waandishi hao.

 «Tunaomba radhi kwa yote yaliyotokea kwenye bunge la mkoa. Nina wapongeza kwa maandamano haya ya amani, na ninaahidi kufanya juhudi zozote za kukamilisha uchunguzi unaoendelea ili kuwapata wahusika”,alisema.

Katika ripoti yake iliyotolewa mwezi mmoja uliopita, shirika la utetezi wa haki za wapashahabari JED mjini Kinshasa limesema tangu mwanzo wa mwaka huu 2021 limerekodi visa 110 vya udhalilishaji wa wanahabari. Shirika limeitaka serikali ya Congo kujihusisha zaidi katika kushughulikia ukatili dhidi ya wapasha habari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW