1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandishi wawili wakamatwa nchini Ethiopia

1 Julai 2022

Waandishi habari 2 raia wa Ethiopia wanaofanya kazi katika kituo cha mtandao wa YouTube cha Ethio-Forum wamekamatwa, mmoja wao amekamatwa tena siku chache tu baada ya kuachiwa kufuatia kuzuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja

Visuelle Journalisten in Nahost & Afrika | Kameramann beim NY-Forum Africa
Picha: Godong/picture alliance


Haya ni kwa mujibu wa rafiki ya waandishi hao wa habari. Rafiki huyo ambaye hakutaka kutajwa jina ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa mwasisi wa kituo hicho Yaysewe Shimelis alikamatwa nyumbani kwake na karibu maafisa 4 wa polisi waliokuwa hawakuvalia sare rasmi mapema Jumatatu na kufikia sasa hajulikani alipo.

Mwengine aliyekamatwa kutoka nyumbani kwake ni Abebe Bayu ambaye ni mwandishi wa zamani wa televisheni ambaye kwa sasa hajulikani alipo pia.

Kamati ya kuwalinda waandishi wa habari CPJ inasema tangu mwaka 2020, Yaysewe amekamatwa zaidi ya mara tatu ikiwemo katikati ya mwaka 2021 alipowekwa kizuizini kwa katika kambi ya kijeshi eneo la Afar.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW