1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa AU wakosoa uchaguzi mkuu wa Tanzania

6 Novemba 2025

Waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika wamebainisha kwamba uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29.2025 haukuzingatia viwango vya demokrasia.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 29.10.2025
Waangalizi wa Umoja wa Afrika wameukosoa uchaguzi mkuu uliofanyika Tanzania 29.10.2025Picha: Marco Longari/AFP

Waangalizi hao wamebainisha kuwa uchaguzi huo haukuzingatia pia kanuni za Umoja wa Afrika na viwango vingine vya kimataifa vya uchaguzi wa kidemokrasia.

Aidha wametaja kuwepo kwa matukio ya udanganyifu ikiwemo kujazwa kura zisizo halali ndani ya masanduku katika vituo kadhaa vya kupigia kura. Vilivile ripoti hiyo imesema waangalizi wake walishuhudia watu wakipewa karatasi nyingi za kupigia kura na wengine waliruhusiwa kupiga kura bila kuonesha vitambulisho.

Maandamano, vurugu vyatajwa katika ripoti ya waangalizi

Ripoti ya waangalizi hao imeeleza pia juu ya kuwepo kwa maandamano ya vurugu, milio ya risasi, kufungwa kwa barabara, na kuchomwa kwa matairi katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kagera, Dodoma, Kigoma, Tabora, Buhungwa, Singinda. Umoja wa Afrika umeitaka Tanzania kuyapa kipaumbele mageuzi ya sheria za uchaguzi na kisiasa ili kushughulikia sababu kuu za changamoto zake za kidemokrasia na uchaguzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW