Waangalizi waendelea kumiminika kushuhudia uchaguzi Zimbabwe
26 Juni 2018Matangazo
Msemaji wa polisi, Charity Charamba, alisema jana kwamba mripuko huo ambamo Rais Emmerson Mnangagwa alinusurika katika mkutano wa hadhara mwishoni mwa wiki mjini Bulawayo ulisababisha watu wawili kuuwawa.
Waangalizi kutoka nchi 46 na mashirika 15 ya kikanda na kimataifa wanatarajiwa kuangalia uchaguzi huo wa rais na bunge uliopangwa kufanyika Julai 30.
Uchaguzi wa rais unawakutanisha Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 wa chama tawala cha ZANU-PF dhidi ya chama cha muda mrefu cha upinzani cha MDC ambacho mgombea wake ni Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 40.
Uchunguzi wa maoni unaonesha uwezekano wa kuwepo na ushindani mkubwa.