Waasi 6 wa PKK wauwawa Sirnak
26 Desemba 2007Matangazo
ANKARA
Waasi 6 wa chama cha wafanyikazi wa kikurdi cha PKK wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na jeshi la Uturuki karibu na mpaka wa Irak.Opresheni hiyo ya kijeshi katika eneo la milimani la Sirnak imefanyiwa sambamba na mashambulio ya angani yaliyofanywa leo na Jeshi la Uturuki yaliyolenga kambi za PKK huko kaskazini mwa Iraq.Uturuki imethibitisha taarifa kwamba ndege zake za kivita zimeshambulia kwa mara nyingine leo hii kaskazini mwa Iraq kuwalenga waasi hao wa chama cha PKK.Kufikia sasa waasi 11 wa PKK wameuwawa katika mashambulio yaliyoanza tangu jana.