1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Niger wanaotaka kuachiliwa kwa Bazoum wajisalimisha

12 Novemba 2024

Maafisa katika eneo la kaskazini la nchi inayotawaliwa kijeshi ya Niger, wamesema kuwa wanachama tisa wa vuguvugu la waasi wanaotafuta kuachiliwa kwa rais wa nchi hiyo aliyeondolewa mamlakani, wamejisalimisha.

Mohammed Bazoum | Niger
Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohammed BazoumPicha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Kundi la waasi la Patriotic Liberation Front FPL lilianzishwa mwezi Agosti mwaka 2023, mwezi mmoja baada ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia wa Niger Mohamed Bazoum kuondolewa katika mapinduzi ya kijeshi.

Tangu wakati huo, Bazoum amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani yeye na mkewe katika mji mkuu wa Niamey. 

Bazoum afutiwa kinga ya rais na utawala Niger

Afisa mmoja kutoka mkoa wa kaskazini mwa jangwa karibu na Libya amelieleza shirika la habari la AFP kwamba wapiganaji tisa wa FPL walisalimisha silaha katika hafla iliyofanyika jana Jumatatu.

Awali kiongozi wa FPL Mahmoud Sallah alipokonywa kwa muda uraia wake pamoja na wanachama saba wa utawala wa Bazoum ambao walishukiwa kufanya mashambulizi ya kigaidi.