1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi na jeshi wakabiliana Congo, M23 iko tayari kuondoka

7 Desemba 2022

Makabiliano yalizuka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapo jana kati ya wanajeshi wa Congo na vuguvugu la M23, huku waasi hao wakisema wako tayari kujiondoa katika maeneo wanayoyadhibiti.

Mai-Mai Milizen im Kongo
Picha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Askari wa Congo walilikabili kundi hilo nje ya mji wa Bwiza, karibu kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu wa mkoa Goma. Duru zinasema makabiliano hayo yalisababisha wakaazi kukimbia na shughuli katika mji jirani wa Kitchanga kusitishwa.

Machafuko hayo ya karibuni katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita yanajiri wiki moja baada ya shambulizi lililodaiwa kufanywa na M23 mashariki mwa mkoa wa Kivu Kaskazini kuwauwa karibu watu 300, karibu wote wakiwa ni raia.

Waasi hao wametoa taarifa wakisema wako tayari kujiondoa, ikiwa ni sharti muhimu lililowekwa na Angola kwenye mazungumzo ya amani mwezi uliopita pamoja na nchi jirani Rwanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW