1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Waasi wa Houthi wa Yemen wazilenga meli za Marekani

13 Novemba 2024

Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wametumia droni na makombora kuzilenga meli mbili za kivita za Marekani zilipokuwa zikivuka kwenye Ujia wa Bab al-Mandab.

USS Theodore Roosevelt
Picha ikionyesha moja ya manowari ya kijeshi ya Marekani ya USS Theodore Roosevelt iliyochukua nafasi ya USS Dwight D. Eisenhower katika kampeni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya waasi wa Houthi wa Yemen. Picha: Seaman Ryan Holloway/AP/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Jenerali Pat Ryder amethibitisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari jana Jumanne na kuongeza kuwa walifanikiwa kuyazuia mashambulizi hayo.

Hakuna meli iliyoharibiwa wala mtu aliyeumia.

Tangu Novemba, 2023 waasi wa Houthi walianza kuzishambulia meli hizo kwenye Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden wakidai kulipiza kisasi kufuatia vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW