1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi wadai wanakombora lenye kasi ya juu

14 Machi 2024

Waasi wa Houthi Yemen wanadai wanakombora jipya lenye kasi ya juu katika hifadhi yao ya zana. Haya yameripotiwa na shirika la habari la Urusi, RIA, lililomtaja afisa mmoja ambaye hakutajwa jina

Jemen I Houthi
Waasi wa Houthi nchini Yemen Picha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Ripoti hiyo pia haikutoa ushahidi wa kuunga mkono madai hayo. Madai haya ya Wahouthi yanaongeza hatari inayoweza kutokana na mashambulizi yao ya meli katika Bahari ya Shamu na njia nyengine za baharini, wakati ambapo Israel inaendeleza mashambulizi yake dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Marekani yashambulia maeneo ya Wahotuhi wa Yemen

Kwa wiki kadhaa sasa Wahouthi wamekuwa wakidokeza kwamba wanapanga kufanya mambo ya kushtukiza katika mapambano hayo ya baharini kwa ajili ya kukabiliana na Marekani na marafiki zake, ambao kwa sasa wamefanikiwa kudengua kombora au droni yoyote yenye bomu inayokaribia meli zake. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW