1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Waasi wa Houthi wakamata eneo la serikali

8 Desemba 2025

Kundi la waasi kusini mwa Yemen limekamata eneo kubwa la serikali inayotambuliwa kimataifa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya visima vya mafuta na kuibua kitisho kipya cha machafuko, miaka kadhaa baada ya mapigano kupungua.

Yemen Sanaa 2025 | Wafuasi wa Houthi waandamana dhidi ya Marekani na Israel
Wanamgambo wa Houthi wakiwa wamelishikilia bango linaloonyesha viongozi wa IranPicha: Osamah Abdulrahman/AP/picture alliance

Baraza la Mpito upande wa Kusini mwa nchi au STC, linaloungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, lilidhibiti eneo la mashariki la Hadramout wiki iliyopita.

Lakini katika kile ambacho hakikutarajiwa, vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia vilijiondoa katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta bila upinzani mkubwa, hii ikiwa ni kulingana na mashahidi.

Utulivu wa kiasi wa miaka ya karibuni uliibua matumaini ya amani kati ya waasi wa Houthi wanaodhibiti maeneo yenye watu wengi zaidi, kaskazini mwa taifa hilo na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia na kutambuliwa kimataifa, iliyoko eneo la kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW