1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Wahouthi wawashikilia wafanyakazi 20 wa Umoja wa Mataifa

20 Oktoba 2025

Waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran wanawashikilia wafanyakazi wapatao 20 wa Umoja wa Mataifa, baada ya kuvamia kituo kingine cha taasisi hiyo ya kimataifa katika mji mkuu wa Yemen - Sanaa.

Sanaa 2025 | Wapiganaji waKihouthi wa Yemen wakiwa katika maandamano
Wapiganaji waKihouthi wa Yemen wakiwa katika maandamano mjini SanaaPicha: Osamah Yahya/dpa/picture alliance

Ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini  Yemen , imesema wafanyakazi hao akiwemo mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF nchini Yemen, wanazuiliwa katika kituo kilichopo katika kitongoji cha Hada kusini magharibi mwa mji wa Sanaa.

Umoja wa Mataifa umesema unawasiliana na kundi hilo la waasi pamoja na wadau wengine ili kujaribu kutafutia suluhu tatizo hilo na kurejesha udhibiti kamili wa vituo vyake huko Sanaa.

Waasi wa Kihouthi  wamekuwa wakiwashutumu bila ushahidi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuwa majasusi wa Marekani na Israel, shutuma zinazokanushwa na Umoja wa Mataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW