1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 waudhibiti mji muhimu wa Kalembe wilayani Masisi

21 Oktoba 2024

Wapiganaji wa kundi la M23 wameuteka tangu hapo jana Jumapili mji muhimu wa Kalembe wilayani Masisi na kusonga mbele hadi wilaya jirani ya Walikale mkoani kivu kaskazini.

Waasi wa M23
Waasi wa M23Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Kuchukuliwa kwa mji huo kumewapa sasa nafasi kubwa waasi hao kuviteka vijiji vyenye utajiri mkubwa wa madini wilayani Walikale. 

Mji huo wa Kalembe unaochukuliwa kuwa njia muhimu ya kuelekea katika wilaya yenye madini ya Walikale, umekumbwa na ghasia tangu mwaka wa 2021 wakati M23 ilipoanzisha tena mashambulizi katika mkoa huu wa Kivu Kaskazini.

Taarifa zinasema kuwa wapiganaji wa kundi la M23 walizilenga kwa makombora ngome za vijana wapiganaji wazalendo alfajiri ya jana Jumapili. hali ambayo ilizua hofu kwa maelfu wa raia waliokimbilia katika vijiji jirani vilivyopo umbali wa kilomita chache kutoka eneo la mapigano.

Watu waliokimbia makazi yao Kongo sababu ya vitaPicha: ALEXIS HUGUET/AFP

Mashirika ya kiraia, hata hivyo, yamesema yana na wasiwasi kutokana na kusonga mbele kwa waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na jeshi la Rwanda na ambao sasa wanasonga kwa kasi kwa kuviteka vijiji wilayani Walikale. Tobi Kahangu ni kutoka shirika la raia wilayani Masisi na amesema kuwa "Hili ni tatizo kubwa kuwaona wananchi wakisumbuliwa na vita hata sehemu walikokimbilia na bila ya serikali kutolinda maeneo yanayowapokea wakimbizi. Tunatizama kwamba waasi wa M23 wanasonga mbele na kupangilia kuviteka vijiji zaidi katika eneo letu ".Vita nchini Kongo imezua mzozo mbaya wa afya ya akili na msaada ni mdogo mno

Asubuhi ya Jumatatu, mamia wa raia wengine wameonekana kwenye barabara toka Kalembe kuelekea mji mkuu wa wilaya hiyo ya Walikale wakibeba mizigo na mifugo lakini wakiwa wamekosa maji na chakula, ameelezea afisa huyo, "Hali ya maisha yaendelea kuwa mbaya sababu ya kukimbia kila siku, hakuna chakula hasa zaidi wakongwe hawana dawa na sehemu ya kulala."

Vyanzo visivyoegemea upande wowote vimebaini kuwa watu wasiopungua 14 wamejeruhiwa katika mapigano hayo  yaliliyolipatia kundi hilo udhibiti wa mji huo muhimu unaoziunganisha wilaya za Masisi, Rutshuru na Walikale.

Wapiganaji wa APCLS, kundi la Maimai  lililokuwa na udhibiti wa Kalembe, wamekimbilia kwenye milima  huku milio ya silaha ikisikika hadi leo asubuhi.

Ufafanuzi: Nani yupo nyuma ya mzozo wa Kongo?

02:01

This browser does not support the video element.

Wakati huo huo, wanaharakati wa haki za binaadamu wamesema waan hofu kufuatia hali mbaya ya kiutu katika eneo hilo lenye vurugu ambamo safari za misaada ya kiutu zimepungua. kama anavyobaini Kusudi Mapendo kutoka shirika la CADH .

"Sisi kama watetezi wa haki za binaadamu tunahofia saana maisha ya wananchi katika eneo la Kalembe sababu njia zote zinazo elekea huko zimefungwa nakuyafanya maisha kuwa magumu zaidi".

Haya yanajiri wakati huu juhudi za kutafuta amani kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo zikifanana kutopata mafanikio makubwa  wakati huu ambamo vita vikisambaa kote mkoani Kivu Kaskazini huku Rwanda ikituhumiwa kuliunga mkono kundi la M23.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW