1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Syria waingia mji wa Hama

6 Desemba 2024

Waasi nchini Syria wameingia kwenye mji wa Hama na kuwalazimisha wanajeshi wa serikali kuondoka na kujipanga nje ya mji huo ambao ulikuwa unashikiliwa na vikosi vya serikali kwa zaidi wa muongo mzima sasa.

 Hama 2024 | Syria
Waasi wa Syria wakiwa kwenye viunga vya mji wa Hama baada ya wanajeshi wa serikali kuondoka.Picha: Ghaith Alsayed/dpa/AP Photo/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya Syria ilisema hapo jana kwamba kumekuwapo na makabiliano makali kati ya jeshi na wale iliowaita magaidi, lakini magaidi hao walifanikiwa kujipenyeza kwenye mji huo muhimu.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, jeshi liliamriwa kuondoka na kujipanga sehemu nyengine ili kuepuka mauaji ya raia wasiokuwa na hatia.

Soma zaidi: Nani anadhibiti eneo gani nchini Syria?

Kwa siku kadhaa sasa, waasi na wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana kwenye mji huo wenye wakaazi milioni moja.

Hama ni mji wa pili mkubwa kutwaliwa na waasi kufuatia uvamizi wao wa ghafla ulioanza wiki iliyopita, ambapo pia wameutwaa mji muhimu wa kaskazini magharibi, Aleppo.

Mkuu wa shirika linalofuatilia vita vya Syria, Rami Abdel Rahman, amesema waasi hao wamewafungulia mamia ya wafungwa, wengine wakiwa wamekaa jela tangu mwaka 2011.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW