1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Syria waiteka kambi ya kijeshi

Josephat Nyiro Charo19 Novemba 2012

Waasi wa Syria wamesema leo (19.11.2012) kwamba wameiteka kambi kubwa ya jeshi kwenye barabara kuu kati ya mji wa Aleppo na mpaka na Uturuki.

A Syrian rebel fighter takes aim at government forces, from a flat in a rebel controlled building on the front line in Aleppo's northern Izaa quarter, on November 3, 2012. Syrian rebels said they had launched a major assault on a northern airbase used to deploy regime air power, on the eve of a crucial meeting to decide the future of the opposition. AFP PHOTO/PHILIPPE DESMAZES (Photo credit should read PHILIPPE DESMAZES/AFP/Getty Images)
Syrien Aleppo Bürgerkrieg RebellenPicha: AP

Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limetoa mkanda wa video unaoonyesha waasi wakiwa ndani ya kambi ya Orum al-Sughra katikati ya vifaru na silaha walizokuwa wameziteka. Kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, wanajeshi wasiopungua 25 walio watiifu kwa rais wa Syria, Bashar al Assad, wamechukuliwa kama wafungwa wa kivita.

Taarifa ya shirika la habari la Aleppo imesema vifaru takriban 15 vimetekwa. Mwanaharakati wa upinzani katika eneo la kaskazini la Syria, Mohammad Abdallah, amesema silaha zilizokuwa katika kambi hiyo zilikuwa zikitumiwa kufanyia mashambulizi ya mabomu katika miji na vijiji katika viunga vya mji wa Aleppo na mkoa jirani wa Idlib. Kambi hiyo inapatikana kilometa 25 magharibi mwa Aleppo, kati ya mji huo na mpaka na Uturuki.

Upinzani wa Syria umetuma pia mkanda wa video ukionyesha mapambano makali karibu na kambi ya jeshi ya Nairab mjini Aleppo, mkoa wa mashariki wa Deir al Zour na maeneo ya viunga vya mji wa Damascus.

Uholanzi na Ujerumani kuisaidia Syria

Wakati huo huo, Uholanzi na Ujerumani zinatafakari kuipelekea Uturuki makombora kuisaidia kuulinda mpaka wake na Syria. Uturuki imesema imefanya mazungumzo na washirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO kuhusu njia ya kuimarisha usalama katika mpaka wake wa kilometa 900 na Syria baada ya makombora kuanguka katika himaya yake kutoka Syria.

Waziri wa ulinzi wa Uholanzi, Jeanine Hennis-Plasschaert, amesema jumuiya ya NATO haipo kufanya kazi bure. Shirika la habari la ANP nchini Uholanzi limemnukulu waziri huyo akisema Uturuki haijawasilisha ombi rasmi lakini Uholanzi na Ujerumani ndizo nchi zenye wazalendo barani Ulaya. Shirika la ANP limesema waziri Jeanine alijadiliana na mwenzake wa Ujerumani wiki iliyopita kuhusu uwezekano wa kuisaidia Uturuki.

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuijadili Syria

Hii leo mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu masuala tete katika eneo la Mashariki ya Kati, lakini vile vile kutofuata mkondo wa Ufaransa kuutambua rasmi upinzani mpya wa Syria. Umoja huo kwa muda mrefu umetoa mwito vuguvugu la upinzani liungane kumuondoa madarakani rais wa Syria, Bashar al Assad.

Bashar al-AssadPicha: AFP/Getty Images

Kwenye ujumbe wake wa leo makundi makubwa ya waasi wa kiislamu mkoani Allepo, yakiwemo Al-Nusra Front na Liwa al-Tawhid, yameukataa muungano mpya wa upinzani, yakisema yanataka taifa la kiislamu.

Urusi yalaumiwa

Kwa upande mwingine Canada imeinyoshea kidole cha lawama Urusi kwa kutofanya lolote kuisaida Syria huku nchi hiyo ikitumbukia katika matatizo mazito. Waziri wa ulinzi wa Canada, Peter McKay amesema mwishoni mwa mkutano wa kimataifa wa usalama uliofanyika jana huko Halifax kwamba Urusi inalazimika kufanya mengi zaidi.

Mwandishi: Josephat Charo/RTRE/APE

Mhariri: Sekione Kitojo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW